Pata taarifa kuu
BURUNDI-TANZANIA-WAKIMBIZI-USALAMA

Kundi la kwanza la wakimbizi wa Burundi waishio Tanzania kuwasili Alhamisi

Wakimbizi wa Burundi katika eneo la Kagunga, kwenye Ziwa Tanganyika, upande wa Tanzania.
Wakimbizi wa Burundi katika eneo la Kagunga, kwenye Ziwa Tanganyika, upande wa Tanzania. REUTERS/Thomas

Burundi inasema kundi la kwanza la wakimbizi ambao wamekuwa wakiishi katika nchi jirani ya Tanzania, wataanza kurejeshwa nyumbani siku ya Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Nestor Bimenyimana, Afisa wa juu wa serkali ya Burundi anayehusika na mradi wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi, ameliambia Shirika la Habari la Uingereza la Reuters kuwa mpango huo utaanza kutekelezwa baada ya makubaliano ya serikali yake na Tanzania.

Aidha, amesema kuwa kundi la kwanza, litawajumuisha wakimbizi 1,000 ambao Bimenyimana, amesema wanaorudi, na ambao wanafanya hivyo kwa hiari yao.

Serikali za Burundi na Tanzania mwezi Agosti, zilikubaliana kuwa wakimbizi zaidi ya 200,000 ambao wamekuwa wakiishi nchini Tanzania wataanza kurudi nyumbani kuanzia tarehe 1 mwezi Oktoba.

Idhaa ya Kiswahili ya RFI imejaribu kumpigia simu Waziri wa Mambo ya ndani wa Tanzania Kangi Lugola, kumuuliza kuhusu mchakato huu, lakini hakuweza kupokea simu.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR na mashirika mengine ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu, yameeendelea kutoa wito kwa Tanzania na Burundi kutowalizimisha wakimbizi hao kurudi nyumbani kwa nguvu.

Idadi kubwa ya wakimbi hao walikimbilia nchini Tanzania mwaka 2015, baada ya mzozo wa kisiasa katika nchi yao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.