Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA-MAZINGIRA-UTAFITI

Umasikini Unachangia kuzorota kwa Ukuaji wa Miji Afrika

Jiji la Dar es salaam
Jiji la Dar es salaam www.nationalgeographic.com/

Kasi ya kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na usimamizi mbovu wa mipango miji ni miongoni mwa sababu zinazochangia ujenzi holela nchini Tanzania na hivyo kuathiri Maendeleo ya Ukuaji wa Miji.

Matangazo ya kibiashara

Katika Kongamano la Kuadhimisha siku ya Ukuaji wa miji kati ya Tanzania na Ufaransa Naibu waziri wa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mwita Waitara anasema lazima mipango izingatiwe ili kufikisha huduma muhimu kwa wananchi.

Akifungua kongamano hilo Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira George Simbachawena amesema Jiji la Dar es Salaam linatajwa kuwa Miongoni mwa majiji yanayokua kwa kasi Barani Afrika, baada ya Abuja nchini Nigeria na Kinsasa nchini DRC Hivyo serikali ya Tanzania inachukua hatua za kuweka mipango miji

"Bila kuzingatia mipango miji uchumi wa watu wetu utachangia kuongezeka kwa Uharibifu wa Mazingira, hivyo ni lazima tuchukue hatua stahiki,'"alisema Simbachawene

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti na kupunguza umasikini nchini Tanzania (REPOA) anasema Umasikini unachangia kwa asilimia kubwa kutotekelezeka kwa mipango miiji

Serikali ya Ufaransa imekuwa ikiisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni chachu ya ukuaji wa Uchumi, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier anasema lengo ni kutafuta ufumbuzi,kongamano hilo ni mwanzo

''Maazimio ya Kongamano hili yatajadiliwa katika Mkutano wa Ufrika utakaofanyika nchini Ufaransa June 2020,' alisema Clavier.

Ifikapo Mwaka 2030 Jiji la Dar es salaam linakadiriwa kuwa na watu zaidi ya Milioni 10.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.