Pata taarifa kuu
TANZANIA-NYERERE-KIFO-KIGODA

Brigedia Mkelemi: Nyerere alikuwa nguzo ya ulinzi na usalama wa Tanzania

Brigedia Jenerali Mbaraka Mkelemy kutoka chuo cha Ulinzi cha Tanzania NDC akiwasilisha mada kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere katika sekta ya ulinzi.
Brigedia Jenerali Mbaraka Mkelemy kutoka chuo cha Ulinzi cha Tanzania NDC akiwasilisha mada kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere katika sekta ya ulinzi. RFI/Fredrick Nwaka

Wakati Tanzania ikijiandaa kuadhimisha miaka 20 tangu kifo cha rais wa kwanza wa taifa hilo, viongozi mbalimbali wameelezamkuwa kiongozi huyo alikuwa nguzo ya ulinzi wa Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Nyerere rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania aliaga dunia Oktoba 14 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza.

Akiungumza katika kongamano la siku mbili la Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Brigedia Mbaraka Mkelemy kutoka Chuo cha Ulinzi cha Tafa (NDC), amesema kiongozi huyo alikuwa mhimili wa usalama wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Mwalimu aliunda Jeshi la wananchi wa Tanzania lenye watalaamu lililokuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa Afrika. Jeshi lina dhamana ya kulinda mipaka na usalama wa nchi yetu,”amesema Brigedia huyo wa Jeshi la Wananchi wa tanzania.

Kuhusu sekta ya afya, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Profesa Lawrence Mseru amesema serikali ya Mwalimu Nyerere ilitoa kipaumbele kwa hudma za afya kwa raia wote.

 

Licha ya kufariki dunia Nyerere anasalia kuwa kiongozi anayependwa na watanzania wengi na alilitawala taifa hilo la Afrika mashariki kutoka mwaka 1961 hadi 1985 alipong'atuka kwa hiari.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.