Pata taarifa kuu
Tanzania-Kenya-Uganda-Rwanda-Burundi

AFD kushirikiana na Hospitali za Umma nchini Tanzania kukabiliana na Magonjwa ya Saratani

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier akizungumza na waziri wa Afya nchini humo Ummy Mwalimu
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier akizungumza na waziri wa Afya nchini humo Ummy Mwalimu Picha;MUHAS

Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD limesema lipo tayari kutoa fedha ili kushirikiana na Hospitali za umma nchini Tanzania katika kukabilaina na magonjwa ya saratani kufuatia ugonjwa huo kuwa wa sita kwa kusababisha vifo nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia mpango huo jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya Huduma za afya ya nchi ya Ufaransa, Mkurugenzi Mkazi wa AFD nchini Tanzania, Stephanie Mouen amesema saratani ni miongoni mwa mnagonjwa yanayosababisha vifo vingi katika nchi zinazoendelea.

   “Saratani ni Ugonjwa wa pili kusababisha vifo kwa nchi zinazoendelea na wa Sita nchini Tanzania ,mradi huu tutatekeleza katika hospitali za Muhimbili,Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na Hospitali ya Bugando”-Alisaema Mouen

Mradi huo utatekelezwa katika Mikoa ya Mwanza na Dar es salaam Dakta Siana Nkya mtafiti kutoka chuo kikuu cha Sayansi na tiba cha Muhimbili NUHAS anasema wananachi wanauelewa mdogo kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza .sasa wanashirikiana na nchi za Ghana na Nigeria kukuza uelewa wa Sikoceli.

Meneja kutoka shirika linalosambaza vifaa tiba katika nchi za Afrika Mashariki la BioMerieux Jackline Karachi amesema Gharama za Kufanya Uchunguzi ni changamoto nyingne katika nchi zinazoendelea, hali inayowalazimu wagonjwa kutumia dawa pasipo kuwanyiwa uchunguzi wa kitabibu na hivyo kusababisha usugu wa dawa na kugonjwa kuleta athari kwa kiwango kikubwa na hivyo kushindwa kupona.

Kwa Upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier anasema nchi za Umoja wa Ulaya ikiwemo Ufaransa zinatoa kipaumbele katika masuala ya afya.

   “ Masuala yanayohusu afya ni masuala muhimu kwa Umoja wa Ulaya na Ufaransa hasa katika kupambana kupunguza vifo kwa wananch”-Alisema Clavier

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.