Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Mustakabali wa kisiasa wa Burundi mashakani

Polisi inanyooshewa kidole cha lawama kwa kuwaunga mkono vijana wa chama tawala, Ibonerakure, kwa kuwanyanyasa wapinzani.
Polisi inanyooshewa kidole cha lawama kwa kuwaunga mkono vijana wa chama tawala, Ibonerakure, kwa kuwanyanyasa wapinzani. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana

Kufuatia visa vya mauaji na mivutano ya kisiasa inayoendelea nchini Burundi, ikiwa imesalia miezi isiozidi saba kabla ya kufanyika uchaguzi wa urais nchini humo, hali ya kisiasa nchini humo inatisha.

Matangazo ya kibiashara

Visa vya kuteketeza kwa moto ofisi ndogo za chama kikuu cha upinzani cha CNL, katika maeneo mbalimbali ya nchi vinaendelea, huku chama hicho kikinyooshea kidole cha lawama vijana kutoka chama tawala, CNDD-FDD, Imbonerakure kuhusika na visa hivyo.

Hata hivyo vuguvugu la vijana hao, ambao Umoja wa Mataifa unalitaja kama kundi la wanamgambo, limefutilia mbali madai hayo na kusema kwamba chama cha CNL kinachoongozwa na mbabe wa zamani wa kivita Agathon Rwasa, kinaendelea kupaka matope vijana wake kwa madai yasiyoeleweka.

Vijana wa chama tawala "Imbonerakure" wakiwa kwenye moja ya maonesho
Vijana wa chama tawala "Imbonerakure" wakiwa kwenye moja ya maonesho RFI

Mapema wiki hii Rais Pierre Nkurunziza alifanya mabadiliko madogo katika idara ya upelelezi na kuwaondoa kwenye nafasi zao za kazi baadhi ya maafisa wa idara hiyo, hali ambayo wengi wanaona kwamba huenda ikachochea mvutano katika kambi ya rais, hasa wakati huu nchi hiyo ikikaribia uchaguzi wa urais.

Wakati huo huo hali ya kisiasa na kibinadamu nchini Burundi inaendelea kutia wasiwasi. Hali ya kibinadamu inazidi kudorora kila uchao, hususan kukamatwa watu kiholela bila kufunguliwa mashtaka, mauaji, watu 180,000 wakisalia wakimbizi wa ndani huku 400, 000 wakisaka hifadhi nje ya nchi.

Katika hitimisho la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Burundi ulioanza tarehe 4 na kumalizika tarehe 7 Juni mwaka huu mjini Gitega, katikati mwa Burundi, baraza hilo lilitoa ujumbe wake ambao kwa hakika unaonesha wasiwasi wa kuongezeka kwa vurugu na ukosefu wa kutovumiliana kisiasa ambapo katika maeneo mengi ya nchi, linasema mivutano hiyo imesababisha mapigano hadi kufikia vifo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.