Pata taarifa kuu
BURUNDI-PIERRE NKURUNZIZA-CNDD-FDD-EVERISTE NDAYISHIMIYE

Jenerali Evariste Ndayishimiye ateuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama tawala nchini Burundi

Jenerali Everiste Ndayishimiye ameteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD
Jenerali Everiste Ndayishimiye ameteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD REUTERS/Evrard Ngendakumana

Chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD kimemtangaza Jenerali Evariste Ndayishimiye kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Matangazo ya kibiashara

Burundi inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Mei mwaka huu na tayari rais wa sasa Pierre Nkurunziza alitangaza kung'atuka uongozini.

Jenerali Ndayishimiye ametangazwa leo baada ya kikao cha ndani kilichofanyika leo jumapili Mjini Bujumbura na kuhudhuriwa na rais anayemaliza muda wake Pierre Nkurunziza.

Ndayishimiye mwenye umri wa miaka 52 ni mshirika wa karibu wa rais Nkurunziza na sasa anaongoza kitengo cha usalama wa kijeshi katika ofisi ya rais na aliwahi kuhudumu kama waziri wa usalama.

Mapema wiki iliyopita chama tawala cha CNDD-FDD kiliridhia kung'atuka kwa rais Nkurunziza aliyetawala taifa hilo amskini tangu mwaka 2005.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.