Pata taarifa kuu
KENYA-MOI-KIFO-WAKENYA

Wakenya kumwaga rais wao wa zamani Daniel Arap Moi kuanzia Jumamosi

Rais wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi
Rais wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi Reuters/George Mulala

Ibada ya wafu kumkumbuka rais wa pili wa Kenya Daniel Torotich Arap Moi, aliyefariki dunia wiki hii jijini Nairobi akiwa na umri wa miaka 95, itafanyika wiki ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa serikali jijini Nairobi  wamesema kuwa, siku ya Jumanne wiki ijayo, itakuwa ni siku ya mapumziko, kutoa nafasi kwa raia wa nchi hiyo kuhudhuria ibada hiyo itakayofanyika katika uwanja taifa wa Nyayo, jijini Nairobi.

Katika hatua nyingine, mwili wa Moi utapelekwa katika majengo ya bunge kuanzia siku ya Jumamosi hadi Jumatatu wiiki, na wananchi watapata fursa ya kumuaga kiongozi wao wa zamani kati ya saa mbili asubuhi na saa 11 alfajiri.

Wakenya wanaendelea na maombolezo ya kitaifa, hadi atakapozikwa kiongozi huyo wa zamani ambaye anakumbukwa kwa njia mbalimbali,  waliompenda wakisema, alikuwa kiongozi shapavu, mkarimu aliyehubiri amani na mshikimano nchini humo.

Wakosoaji wa uongozi wake wanasema alikuwa dikteta.

Moi aliyeongoza Kenya kwa miaka 24 anatarajiwa kuzikwa wiki ijayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.