Pata taarifa kuu
KENYA-MOI-SIASA

Mwili wa Moi kuagwa kwa siku ya tatu na ya mwisho

Rais wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi
Rais wa zamani wa Kenya Daniel Arap Moi Reuters/George Mulala

Wakenya kwa siku ya tatu na ya mwisho leo, wataendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Daniel Torotich arap Moi, aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Mwili wa kiongozi huyo aliongoza Kenya kwa miaka 24, umekuwa ukilazwa katika majengo ya bunge jijini Nairobi kwa siku mbili zilizopita, kutoa nafasi kwa wananchi wa kawaida kuuga.

Shughuli ya kuuaga mwili huo ilianza Jumamosi Februari 8 na kutarajiwa kumalizika leo Jumatatu. Siku ya Jumanne kutafanyika misa kubwa ya wafu katika Uwanja wa Kimataifa wa Moi.

Mazishi ya kiongozi huyo wa zamani, yatafanyika siku ya Jumatano nyumbani kwake huko Kabarak katika kaunti ya Nakuru lakini kesho, kutakuwa na ibada ya kitaifa katika uwanja wa Nyayo, inayotarajiwa kuhudhuriwa pia na marais mbalimbali kutoka barani Afrika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.