Pata taarifa kuu
KENYA-MOI-SIASA

Mazishi ya Moi: Viongozi kutoka Afrika Mashariki wahudhuria ibada ya kitaifa

Mwili wa rais wa aliyekuwa rais wa Kenya Daniel Arap Moi, Februari 11 2020
Mwili wa rais wa aliyekuwa rais wa Kenya Daniel Arap Moi, Februari 11 2020 KBCChannel1

Marais mbalimbali kutoka eneo la Afrika Mashariki wameungana na Wakenya, katika ibada ya kitaifa ya kumuaga aliyekuwa rais wa nchi hiyo Daniel Toroitich Arap Moi, aliyefariki dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95.

Matangazo ya kibiashara

Waombolezaji waliwasili mapema katika uwanja wa taifa wa Nyayo jijini Nairobi kuhudhuria ibada hiyo, katika uwanja huo ulionjegwa na rais huyo wa zamani waKenya.

Jeshi la Kenya, lilihusika pakubwa katika maombolezo hayo, huku bendi ikicheza nyimbo za huzuni.

Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, amemkumbuka rais huyo wa zamani kama mtu aliyependa upendo na amani.

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga alisema kwamba japokuwa mzee Moi alikuwa na makosa alisaidia katika kutengeneza katiba mpya mbali na kuleta elimu kwa wote pamoja na maziwa ya nyayo. Raila alisema kwamba mzee Moi anafaa kukumbukwa kwa mazuri aliyotenda badala ya mabaya anayohusishwa nayo.

Viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika Mashariki nao pia walipata fursa ya kumkubuka Moi, rais Magufuli ambaye hotuba yake ilisomwa na rais mstaafu Benjamin Mkapa akiandamana na mrithi wake Jakaya Mrisho Kikwete alisema kwamba uhusiano mzuri kati ya Kenya na Tanzania umeendelea kuwepo kutokana na uongozi wa rais Moi.

Mkapa alisema kwamba licha ya kufanya kazi na Moi alimtaja pia kama mshauri wake mkuu.

Naye rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba rais mstaafu atakumbukwa kwa mazuri aliyoleta nchini Kenya na eneo la Afrika mashariki kwa ujumla. Alisema kwamba Moi alikuwa dawa ya kenya kwa kuwa aliweza kuliongoza taifa hili bila ya migogoro.

Alisema kwamba hatua yake ya kukiongoza chama cha KADU kufanya muungano na KANU ilikuwa dhihirisho tosha kwamba ni kiongozi aliyetaka mshikamano wa nchi.

Rais wa Rwanda Paul Kagame walimsifu mzee kama kiongozi aliyeunganisha makabila tofauti nchini Kenya na kuleta amani katika eneo zima la Afrika mashariki.

Moi atazikwa kesho nyumbani kwake huko Kabarak katika kaunti ya Nakuru na atakumbukwa kuongoza taifa hilo kwa miaka 24, na licha ya kusifiwa kwa kuleta umoja wa kitaifa nchini Kenya, waliomfahamu zaidi wanakiri kuwa, alifanya makosa mbalimbali kama binadamu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.