Pata taarifa kuu
BURUNDI-AGATHON-RWASSA-SIASA-UPINZANI

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa kuwania urais

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa, ametangaza kuwania urais mwezi Mei 2020
Kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa, ametangaza kuwania urais mwezi Mei 2020 REUTERS/Mike Hutchings

Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi cha CNL kimemteau kiongozi wake Agathon Rwasa kupeperusha bendera ya chama hicho, wakati wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umefanywa na wajumbe wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu wa chama cha CNL uliofanyika siku ya Jumapili jijini Bujumbura.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 56, alianza kupata umaarufu wa kisiasa mwaka 2008 baada ya kurejea nyumbani baada ya zaidi ya miaka 20 kujificha msituni wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Kabla ya kurejea nyumbani, mwaka 2016 kundi lake la waasi la FNL, lilitia saini mkataba wa amani na serikali ya Bujumbura, lakini mwaka 2020, alikwenda tena mafichoni, akihofia kukamatwa kwa madai kuwa alikuwa anapanga kuifanya nchi kutotawalika.

Hata hivyo, mwaka 2015 alichaguliwa Spika wa bunge la Burundi na kuanza kuonesha nia ya kuongoza taifa hilo la Afrika ya Kati.

Rwassa anatarajiwa kupata ushindani kutoka kwa mgombea wa chama tawala CNN FDD Evariste Ndayishimiye, mshirika wa karibu wa rais Pirre Nkurunziza ambaye hatawania urais, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa mihula mitatu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.