Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA-SIASA

Maswali yaibuka baada ya kuonekana kundi lenye silaha karibu na mji wa Bujumbura

Moja ya maeneo ya mji wa Bujumbura.
Moja ya maeneo ya mji wa Bujumbura. AFP/Carl de Souza

Wakazi wa mji wa Bujumbura na vitongoji vyake wanahoji kuhusu kundi moja lenye silaha lililoonekana wiki moja iliyopita karibu na mji huo, huku baadhi wakisema wana hofia usalama wao.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni kundi hilo ambalo linatajwa kuwa ni "kundi la wahalifu wenye silaha" lilikabiliana na vikosi vya usalama katika Mkoa wa Bujumbura vijijini, moja wapo ya ngome kuu za Chama kikuu cha upinzani cha CNL, Magharibi mwa nchi.

Polisi haikutoa dalili zozote zile ili kuweza kutambuwa washambuliaji hao, hali ambayo imeibua maswali mengi ikiwa imesalia miezi michache tu kabla ya uchaguzi wa Mei 20.

Kundi hilo la watu wenye silaha lilionekana kwenye milima inayozunguka mji wa Bujumbura wiki iliyopita, amesema msemaji wa polisi ya Burundi Pierre Nkurikiye, huku akibaini kwamba siku nne baadaye kundi hilo liliangamizwa, baada ya mapigano na vikosi vya usalama.

Wakati viongozi wa eneo hilo walibaini hadi Jumatatu wiki hii kwamba katika mapigano hayo "majambazi kumi na mbili wenye silaha na afisa mmoja wa polisi waliuawa, idadi hii imeongezeka maradufu kulingana na polisi jana Jumanne. Polisi imebaini kwamba, "wahalifu ishirini na mbili wenye silaha" na maafisa wawili wa polisi waliuawa, wauaji wengine sita walikamatwa na silaha zao nyingi pia vilikamatwa amebaini msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye, ambaye ameambatanisha kuonekana kwa kundi hilo na uchaguzi uliopangwa kufanyika ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu.

Lakini wengi wanajiuliza wakati mashahidi na mashirika ya kiraia wanashtumu vikosi vya usalama vikisaidiwa na vijana wa chama tawala "Imbonerakure" ambao Umoja wa Mataifa unawachukulia kama wanamgambo, kuua makumi wa washambuliaji waliokuwa wamekamatwa, lakini viongozi wamekanusha madai hayo.

Kwa upande wake Chama kikuu cha upinzani cha CNL cha Agathon Rwasa, kimeshtumu viongozi wa Mkoa wa Bujumbura vijijini na vikosi vya usalama kuwakamata zaidi ya wafuasi wake thelathini, tangu kuonekana kwa kundi hilo lisilojulikana.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.