Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kenya yafunga mipaka yake na Tanzania na Somalia

Madereva wa malori wanajiandaa kufanya vipimo vya Corona kwenye mpaka wa Namanga kati ya Kenya na Tanzania, huko Namanga, Kenya, Mei 12, 2020.
Madereva wa malori wanajiandaa kufanya vipimo vya Corona kwenye mpaka wa Namanga kati ya Kenya na Tanzania, huko Namanga, Kenya, Mei 12, 2020. REUTERS/Thomas Mukoya

Serikali ya Kenya imepiga hatua katika vita dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kuzuia maambuzi zaidi, amesema Waziri wa Afya Mutahi Kangwe alipohutubia mkutano wa 73 wa kimataifa wa Afya.

Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine waziri Kagwe amesema wataendelea kuwapima madereva kutoka nchini Tanzania katika maeneo ya mipakani ikiwa ni juhudi za kudhibiti maambukizi ya Corona.

Wakati huo huo Kenya imeamua kufunga mipaka yake na Tanzania na Somalia wakati huu nchi hiyo ikiwa na mamabukizi 963.

Kufikia sasa ugonjwa wa Covid-19 umeuwa watu 50 nchini Kenya na wagonjwa 358 wamepona.

Hayo yanajiri wakati Tanzania imeondoa sharti la wageni wanaoingia katika taifa hilo kuwekwa karantini kwa siku 14 ilivyohitajika baada ya mlipuko wa virusi vya Corona.

Serikali kupitia barua ambayo imetiwa saini na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, imesema wageni watakaofika Tanzania watafanyiwa tu vipimo vya Covid 19, wala si kuwekwa karantini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.