Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Hugo Chavez kuendelea na wadhifa wake licha ya kukabiliwa na maradhi yaliyozoresha afya yake

©Reuters.

Serikali ya Venezuela imethibitisha kuwa Rais wa nchi hiyo anayesumbuliwa na maradhi ya saratani Hugo Chavez hataweza kuapishwa tarehe kumi ya juma lijalo kama ilivyopangwa hapo awali, lakini ataendelea kushika wadhifa wake kama kawaida kwani katiba ya nchi hiyo inamtambua kama Rais kutokana na kupata ridhaa ya kura za wananchi.

Matangazo ya kibiashara

Makamu wa Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro amesema kiongozi huyo ataapishwa wakati mwingine kutokana na hali yake kutotengamaa mpaka sasa.

Maduro pia amekataa madai ya wapinzani ya kuitishwa kwa uchaguzi mkuu mwingine ama Rais Chavez kukabidhi madaraka yake kwa Spika wa Bunge la nchi hiyo ikiwa hataapishwa siku iliyopangwa.

Rais Chavez bado yupo nchini Cuba akiendelea kupatiwa matibabu na sasa anasumbuliwa na maradhi ya mapafu ambayo yametokana na oparesheni aliyofanyiwa hivi karibuni ya kuondoa saratani ya ubongo hali ambayo imesababisha apate matatizo ya kupumua.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.