Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-EU

Iran na IAEA zafikia makubaliano kuhusu mpango wa suluhu ya mzozo wa nyuklia

Waziri wa mambo ya Kigeni wa Marekani, John Kerry (kushoto) akiwa kwenye meza ya mazungumzo na ujumbe wa Iran pamoja na Umoja wa Ulaya
Waziri wa mambo ya Kigeni wa Marekani, John Kerry (kushoto) akiwa kwenye meza ya mazungumzo na ujumbe wa Iran pamoja na Umoja wa Ulaya Reuters

Nchi ya Iran na shirika la Umoja wa matiafa linalisimamia matumizi ya nguvu za Atomic duniani IAEA wamefikia makubaliano ya namna ya kufikia suluhu ya mambo ambayo hayakuweza kupatiwa ufumbuzi kwenye mkutano wao wa mjini Geneva uliomalizika hapo jana.  

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa masuala ya Nyukilia nchini Iran, Ali Akbar Salehi amethibitisha kufikiwa kwa makubaliano hayo kati ya nchi yake na mkuu wa shirika la IAEA, Yukiya Amano mjini Tehran.

Makubaliano haya kati ya utawala wa Iran na Shirika la IAEA yanakuja saa chache toka kumalizika kwa mazungumzo ya siku tatu ya mjini Geneva kati ya ujumbe wa Iran na mataifa ya magharibi kuhusu mpango wake wa nyuklia bila ya kufikiwa muafaka.

Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la IAEA, Yukiya Amano anafanya ziara nchini Iran kujaribu kuushawishi utawala wa nchi hiyo kuruhusu waangalizi wa shirika hilo kutembelea baadhi ya vinu ambavyo Iran inatuhumiwa kuvitumia kutengeneza silaha za kemikali.

Makubaliano haya yanatoa nafasi ya kuandaliwa kwa utaratibu wa kupata suluhu ya masuala ambayo yalijadiliwa mjini Geneva na hatimaye kuishuhudia Iran ikipata ushirikiano toka jumuiya ya kimataifa ambayo kwa sasa imeitenga.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry hii leo amesema anafuatilia kwa ukaribu mchakato wa kupatikana kwa suluhu kati ya Iran na mataifa ya magharibi huku akionesha kuridhishwa na namna Iran inavyojitahidi kupata suluhu.

Hata hivyo waziri Kerry ameionya nchi ya Iran kuhusu kujitoa kwenye mazungumzo hayo na kwamba kufanya hivyo kutachochea mzozo zaidi na mataifa ya magharibi ambayo yanashinikiza nchi hiyo iweke wazi mpango wake wa nyuklia.

Katika hatua nyingine, rais wa Iran, Hassan Rowhani amesema nchi yake haitaachana na mpango wa nyuklia licha ya shinikizo toka kwa mataifa ya magharibi kuitaka iachane na mpango huo.

Kwa upande mwingine nchi ya Israel kupitia kwa waziri mkuu wake, Benjamin Netanyahu imesema kuwa haiamini kama Iran itaweza kutoa ushirikiano unaohitajika kwa jumuiya ya kimataifa na kwamba mataifa yanayoendelea na mazungumzo na Iran yamepotoka kwakuwa hawatafikia muafaka.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.