Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-ISRAEL

Marekani na Iran zatupiana lawama kuhusu kukwama kwa mazungumzo ya Geneva

Waziri Kerry akiwa na mkuu wa Sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton na waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Zarif
Waziri Kerry akiwa na mkuu wa Sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton na waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Zarif Reuters

Nchi za Marekani na Iran zimetupiana maneno ya kejeli huku kila mmoja akimlaumu mwenzake kwa kusababisha kushindwa kufikia makubaliano kwenye mazungumzo ya mjini Geneva kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran. 

Matangazo ya kibiashara

Akiwa ziarani kwenye nchi ya Falme za Kiarabu, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ameutuhumu ujumbe wa Iran kwa kusababisha nchi hizo kushindwa kufikia makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Waziri Kerry amesema kuwa Marekani itaendelea kuwalinda nchi washirika wake kwenye eneo la mashariki ya kati dhidi ya vitisho vya nchi ya Iran na mpango wake wa nyuklia ambao unatishia usalama wa eneo hilo.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mjini Abu Dhabi, waziri Kerry amesema nchi ya Iran imeendelea kutoa mapendekezo ambayo hayatekelezeki na wala hayakubaliki kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu namna inataka ishirikiane na jumuiya ya kimataifa kufikia muafaka kwenye suala hilo.

Wakati waziri Kerry akitoa kauli hiyo, waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif akajibu mapigo kwakuuliza kuwa ni nani aliyekwamisha mazungumzo ya mjini Geneva kama sio nchi ya Marekani.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twita, waziri Zarif anasema Marekani isijikoshe kwa jumuiya kimataifa kuituhumu Iran kuwa ilikwamisha mazungumzo ya Geneva wakati ni yenyewe ambayo ilikuja na madai mapya ambayo nchi ya Iran haiwezi kutekeleza kwa shinikizo.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa Marekani inajitetea ili kuionesha Serikali ya Israel kuwa iko pamoja nayo katika kuhakikisha muafaka utakaofikiwa utakuwa wa manufaa kwa nchi zote wanchama za Umoja wa Mataifa na hasa Israel.

Licha ya matamshi ya viongozi hawa, hapo jana shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia nguvu za Atomic IAEA lilitiliana saini na Serikali ya Iran mkataba maalumu utakaowezesha kufikia muafaka kuhusu kufanyika kwa uchunguzi kwenye vinu vyake vya Nyuklia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.