Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Mlipuko mkubwa watokea mbele ya hoteli ya wageni Kabul

Akari polisi wa Afghanistan akitoa ulinzi katika eneo la shambulizi, Agosti 1, 2016.
Akari polisi wa Afghanistan akitoa ulinzi katika eneo la shambulizi, Agosti 1, 2016. REUTERS/Omar Sobhani

Shambulizi kubwa la lori lililokua limetegwa mabomu lililenga usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu hii hoteli ya wageni iliyona ulinzi mkali katika kitongoji cha mji wa Kabul, shirika la habari la AFP limearifu, likinukuu vyanzo vya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Hakuna ripoti yoyote ya majeruhi ambayo imekua imeshatolewa Jumatatu hii asubuhi, lakini kituo cha televisheni cha Tolo chini humo kimearifu kumekua na ufyatulianaji risasi karibu na eneo kulikotokea shambulio hilo, ambapo vikosi vya usalama vimetumwa. Washambuliaji watatu wameuawa wakati wa operesheni ya polisi.

Kundi la Taliban limekiri kuwa kutekeleza shambulizi hilo , likisema kuwa "limelipua lori lililokua limejaa mabomu mbele ya mita kadhaa na hoteli ya Northgate", ilioko kwenye barabara mpya inayoelekea katika kambi ya jeshi la Marekani ya Bagram, kaskazini-mashariki mwa mji wa Kabul. wapiganaji wa kiislamu wameongeza kwenye Twitter kwamba mlipuko huo "umewafungulia njia wapiganaji [wao] walio kuwa na silaha ndogo ndogo katika hoteli hiyo."

Polisi, hata hivyo, ilikataa Jumapili usiku kuthibitisha ukweli wa taarifa hii na kukanusha kuwa kulikuwepo na ufyatulianaji risasi na kundi la washambuliaji katika eneo hilo. Vile vile, Mkuu wa uchunguzi wa jinai katika mji wa Kabul, Feraidoon Obaidi, aliyehojiwa na shirika la habari la AFP, amesema mtu yeyote aliyeuawa wala kujeruhiwa. Eneo lote limezingirwa kwa kuzuiwa mtu yeyote kukaribia hoteli na hoteli yenyewe haisogelewi.

Msemaji wa kundi la Taliban, Zabihullah Mujahid, amesema kuwa "wavamizi wa Marekani zaidi ya mia moja wameuawa na wengine kujeruhiwa" katika operesheni hii tata, taarifa ambayo ni vigumu kuichunguza, na ambayo haijathibitishwa na vyanzo huru.

Operesheni kababmbe la polisi

Baada ya masa saba eneo la tukio likizingirwa, washambuliaji hao watatu dhidi ya hoteli ya Northgate wameuawa kabla hata hivyo kufanya uhalkifu wowote katika hoteli hiyo, afisa wa polisi amebaini. “ Operesheni imemalizika, bila hasara yoyote ndani na nje ya hoteli”, amebaini mkuu wa polisi mjini Kabul, Abdul Rahman Rahimi, ambaye awali alisema kuwa askari polisi mmoja aliuawa na wengine watatu walijeruhiwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.