Pata taarifa kuu

Narendra Modi afanya ziara ya kihistoria nchini Israel

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia) akimkaribisha mwenzake wa India Narendra Modi mjini Tel Aviv, Jumanne, Julai 4, 2017.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia) akimkaribisha mwenzake wa India Narendra Modi mjini Tel Aviv, Jumanne, Julai 4, 2017. REUTERS/Ammar Awad

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi yuko ziarani nchini Israel. Hii ni mara ya kwanza Waziri Mkuu wa India kuzuru nchi hiyo, miaka 25 baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. serikali ya Israel imekaribisha ziara hiyo ikibaini kwamba ni hatua ya kihistoria.

Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka ya 25 ya uhusiano wa kidiplomasia, India na Israel wameendeleza biashara zao kwa wingi na mkakati mbalimbali. India kwa sasa ni moja ya wateja wakuu wa Israel katika sekta ya silaha. Biashara kati ya nchi hizi mbili inatarajiwa kufikia Dola bilioni 5 hadi mwishoni mwa mwaka huu, mwandishi wetu katika mji wa Jerusalem, Guilhem Delteil amearifu.

Kwa upande wake Yuval Rotem, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Israel, amesema ziara hiyo ni ishara kubwa ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. "Hii kwa kweli ni ziara ya kihistoria. Waziri Mkuu ataongozana na Waziri Mkuu Modi katika ziara yake yote hiyo, jambo ambalo si la kawaida katika ziara za kiserikali za miaka ya hivi karibuni. Hii inaonyesha umuhimu ambao tunaona kwa ziara hii, " amesema Bw Rotem.

Narendra Modi hatatozuru Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na walowezi wa Kiyahudi. Haijafahamika iwapo kiongozi huyo wa India atakutana na viongozi wa Palestina.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.