Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Waisrael watatu wauawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Har Adar

Vikosi vya usalama vya Israeli na maafisa wa uokoaji kwenye mlango wa makazi ya walowezi wa Har Adar katika Ukingo wa Magharibi Jumanne, Septemba 26, 2017.
Vikosi vya usalama vya Israeli na maafisa wa uokoaji kwenye mlango wa makazi ya walowezi wa Har Adar katika Ukingo wa Magharibi Jumanne, Septemba 26, 2017. Thomas COEX / AFP

Polisi wa Israel wanasema kuwa mtu mwenye silaha anayejulikana kwa jina la Nimer Jamal, amewaua kwa kuwapiga risasi watu watatu raia wa Israeli karibu na mlango wa eneo la Har Adar katika Ukingo wa Magharib.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yanafanyika wakati mjumbe wa Rais Donald Trump eneo la Mashariki ya Kati Jason Greenblat, akifanya ziara Jerusalem kufufua mazungumzo kati ya Israeli na Palestina.

Mtu mwenye bunduki wa umri wa miaka 37 kutoka aliwapiga risasi walinzi wawili na polisi wa mpaka kwa karibu, na kumjeruhi vibaya mtu mwingine kabla ya kupigwa risasi na vikosi vya usalama.

Mtu huyo anatoka kijiji cha Beit Surik, karibu kilomita mbili mashariki mwa Har Adar.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani mauaji hayo na kusema kuwa mauaji hayo yamesababishwa na uchochezi kutoka upande wa Palestina.

Mazungumzo ya amani kati ya pade hizo mbili yalivunjika mwezi Aprili mwaka 2014, baada ya visa vya mauaji na vitendo vya kikatili kukithiri kutoka pande hizo mbili.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.