Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Antonio Guterres ataka kusitishwa mapigano Yemen

Vita nchini Yemeni vimeua zaidi ya watu 8500 na wengine 49,000 wamejeruhiwa tangu mwezi Machi 2015.
Vita nchini Yemeni vimeua zaidi ya watu 8500 na wengine 49,000 wamejeruhiwa tangu mwezi Machi 2015. AFP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteres ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea nchini Yemen, kati ya vikosi vya serikali na waasi.

Matangazo ya kibiashara

Guteres amesema ni muhimu kwa vita hivyo kukomeshwa kwa sababu ya hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea kushuhudiwa katika mitaa ya jiji kuu Sanaa.

Mapigano makali yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa zilizopita na kusababisha watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa huku walionusurika wakikosa maji, chakula, matibabu na makaazi yao yakiharibiwa.

Magari ya kuwabeba wagonjwa hayawezi kwenda katika maeneo yanayoshuhudiwa mapigano kwa sababu ya usalama wa wafanyakazi wa afya, huku waliojeruhuwa wakishindwa kupata huduma muhimu.

Jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia, limeendelea kupambana na waasi wa Kihuthi na wiki iliyopita, watu zaidi ya 60 wamepoteza maisha kaika mzozo huu ulioanza mwezi Machi mwaka 2015 na kusababisha zaidi ya watu 8,700 kupoteza maisha na Maelfu kuyakimbia makwao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.