Pata taarifa kuu
PALESTINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Mahmoud Abbas amshtumu Trump kwa hatua yake juu ya Jerusalem

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, Januari 5, 2016 Bethlehem.
Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas, Januari 5, 2016 Bethlehem. REUTERS/Ammar Awad

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas amemshutumu rais wa Marekani Donald Trump, na kusema Palestina haiwezi kukubali kamwe Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Matangazo ya kibiashara

Abbas, amesisitiza kuwa Jerusalem ni makao makuu ya kisiasa, kiimani ya Palestina na kumkejeli rais Trump kwa kubadilisha ramani hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hivi karibuni Marekani ilitishia kufunga misaada yake kwa Palestina, huku Palestina ikisema haitakubali kutumiwa na Marekani kutokana na misaada yake. Marekani imekuwa ikitoa msaada wa kifedha kwa Palestina kusaidia kuimarisha usalama.

Wachambuzi wa siasa za eneo la Mashariki ya Kati, wanasema kuwa, tishio hili la Marekani ni kujaribu kuilazimisha Palestina kuja kaatika meza ya mazungumzo na Israel.

Marekani imekuwa ikitoa msaada huo wa kifedha kusaidia kuimarisha usalama lakini pia, kuendeleza maendeleo mbalimbali ya kiuchumi.

Palestina imekuwa ikisema kuwa Marekani kwa kutoa tangazo hilo, haiwezi kuwa msuluhushi asipendelea upande mmoja katika harakati za kutafuta suluhu ya mzozo kati yake na Israel.

Uhusiano kati ya Marekani na Palestina, umedorora baada ya rais Trump, kutangaza kutambua mji wa Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.