Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-USALAMA

Uturuki yaimarisha ulinzi kaskazini mwa Syria

Magari ya kijeshi ya Uturuki yakipiga kambi kwenye mpaka na Syria, Januari 21, 2018.
Magari ya kijeshi ya Uturuki yakipiga kambi kwenye mpaka na Syria, Januari 21, 2018. Caglar Ozturk/Dogan News Agency via REUTERS

Uturuki imetuma wanajeshi wake Kaskazini mwa Syria katika operesheni ya kupambana na wapiganaji wa Kikurdi.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Uturuki inasema kuwa, wapiganaji hao ni magaidi na ni hatari kwa usalama wa nchi yake.

Wapiganaji hao wanaofahamika kama YPG, ngome yao kuu ni Afrin karibi sana na Uturuki.

Kumeshuhudia makabiliano makali kati ya wanajeshi wa Uturuki na wapiganaji hao, huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea kwa maafa zaidi.

Uamuzi huu wa Uturuki huenda ukazua mgogoro kati yake na Marekani ambao inawaunga mkono wapiganaji hao kwa kile inachosema kuwa inasaidia katika vita dhidi ya Islamic State nchini Syria.

Serikali ya Syria inasema Uturuki haikuwaambia kuhusu, operesheni hiyo licha ya serikali ya Ankara kusema kuwa ikuwa imeiambai serikali ya Damascus.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.