Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANI-SAUDI ARABIA-JAMAL-HAKI

Rais wa Uturuki aapa kuweka wazi mauaji ya Khashoggi

Picha ya CCTV ikimuonyesha Jamal Khashoggi akiwasili kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, Istanbul, Uturuki, Oktoba 2, 2018.
Picha ya CCTV ikimuonyesha Jamal Khashoggi akiwasili kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, Istanbul, Uturuki, Oktoba 2, 2018. Demiroren News Agency / AFP

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumanne wiki hii ataweka wazi bila kuficha chochote, alivouawa Mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi, katika ubalozi wa nchi yake jijini Instanbul zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya rais Erdogan imekuja wakati huu Saudi Arabia ikisema haifahamu mwili wa Khashoggi uko wapi, huku Mwana Mfalme Mohammed bin Salman akisema hakufahamu mpango wowote wa kumuua.

Waziri wa Mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir, ameelezea kilichotokea kama mauaji, yaliyotokea kimakosa na kuwashtumu waliomvamia Khashoggi kama watu waliokwenda nje ya mipaka yao.

Hivi karibuni Marekani ilitishia kuvunja uhusiano na Saudi Arabia ikiwa kweli itadhihirika kwamba nchi hiyo ilihusika kwa kifo cha mwaandishi huyo wa habari wa gazeti la Washington Post, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa Saudi Arabia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.