Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAQ-USALAMA

Rais wa Marekani afanya ziara ya kushtukiza Iraq

Rais Trump akitoa hotuba kwa askari wa Marekani wa kambi ya wanaanga ya Al-Asad nchini Iraq, Desemba 26, 2018.
Rais Trump akitoa hotuba kwa askari wa Marekani wa kambi ya wanaanga ya Al-Asad nchini Iraq, Desemba 26, 2018. REUTERS/Jonathan Ernst

Rais wa Marekani Donald Trump amefanya ziara ya kushtukiza nchini Iraq na kukutana na wanajeshi wa taifa lake wanaopambana na kundi la Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Trump ametetea uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini Syria na kusema hili litafanya kwa utaratibu lakini akasisitiza kuwa hana mpango wa kuwaondoa wanajeshi nchini Iraq.

Rais na Mkewe wamekwenda Iraq jioni ya siku ya Krismasi kutembelea askari wetu na wakuu wa kijeshi kuwashukuru kwa kujitolea, kufanikiwa pakubwa katika operesheni zao na kuwataka Siku Kuu njema ya Krismasi na heri ya Mwaka Mpya 2019, " msemaji wa White House, Sarah Sanders ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais wa Marekani aliwasili saa 7:16 jioni saa za Iraq kwenye kambi ya jeshi la wanaanga la Marekani ya al-Assad, ambako alikutana kwa mazungumzo na askari pamoja na wakuu wa kijeshi. Ziara hiyo iliyofanyika kwa siri kwa sababu za kiusalama, imetokea wiki moja baada ya Donald Trump kutangaza hatua ya kuwaondoa askari wa Marekani nchini Syria.

Rais wa Marekani amerejelea kauli yake ya hivi karibuni kuhusu uamuzi wake: "Marekani haiwezi kuendelea kuwa polisi wa dunia," akisema kuwa kundi la Islamic State "limeshindwa kabisa."

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.