Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-USALAMA

Roketi zarushwa tena kuelekea Israeli

Askari wa Israeli wakirusha kombora nje ya ukanda wa Gaza Julai 31, 2014.
Askari wa Israeli wakirusha kombora nje ya ukanda wa Gaza Julai 31, 2014. REUTERS/Baz Ratner

Hali ya sintofahamu imeendelea Jumanne usiku baada ya roketi kurushwa tena kutoka upande wa Ukanda wa Gaza kuelekea Israeli wakati hali ya utulivu imekuwa imerejea Jumanne mchana.

Matangazo ya kibiashara

Mapema Jumanne mchana jeshi la Israeli, Tsahal (IDF) lilijibu kwa mfululizo wa mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za Hamas katika Ukanda wa Gaza, ambapo Wapalestina watano walijeruhiwa. Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ambaye anawania muhula mwingine katika uchaguzi wa wabunge wa Aprili 9, ameagiza pia kupelekwa kwa idadi kubwa ya askari kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza.

Jumanne jioni, kundi la Hamas, ambalo linatawala katika Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007, na makundi kadhaa yanayo bebelea silaha katika eneo hilo yalitangaza katika taarifa yao kwamba usuluhishi wa Misri umepelekea kusitisha mapigano, lakini jeshi la Israeli limeendelea mashambulizi yake ya angani.

Hata hivo mashahidi wanasema hali ya utulivu hatimaye imerejea tangu mapema asubuhi na hatua za usalama kwenye mpaka zimefutwa.

Chanzo cha kijeshi kutoka Israeli kinasema kuwa ndege ya jeshi la Israeli imeendelea na mashambulizi ya anga yalikelenga ngome za kundi la Hamas, baada ya roketi kadhaa kurushwa tena nchini Israeli.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.