Pata taarifa kuu
SYRIA-IRAQ-IS-USALAMA

Kiongozi wa IS al-Baghdadi aonekana kwenye mkanda wa video baada ya miaka 5

Kundi la IS limetoa kanda ya video ya mtu linayedai kuwa kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi, Aprili 29, 2019.
Kundi la IS limetoa kanda ya video ya mtu linayedai kuwa kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi, Aprili 29, 2019. AFP / AL-FURQAN MEDIA

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 5, Kundi la Islamic State limetoa kanda ya video ya kiongozi wake, Abu Bakr al-Baghdadi akikiri kushindwa kwa wapiganaji wake kwenye mji wa Baghuz nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Al-Baghdad anayesakwa na jumuiya ya kimataifa, mara ya mwisho alionekana mwaka 2014 ambapo alitangaza kuzaliwa kwa utawala wa Caliphate kwenye nchi za Syria na Iraq.

Katika mkanda huo wa video Abu Bakr al-Baghdadi, ameapa kulipiza kisasi kwa kupoteza himaya yake.

Baghdadi amesema kuwa shambulio la Jumapili ya Pasaka nchini Sri Lanka lilikuwa shambulio la kulipiza kisasi baada ya kundi hilo kupoteza mji wa Baghuz nchini Iraq.

“Nimeahidiwa kuungwa mkono na wapiganaji wa Burkina Faso na Mali na mazungumzo kuhusu maandamano ya Sudan na Algeria, “ Abu Bakr al-Baghdadi ameongeza, huku akibaini kwamba vita vya kijihad ndio suluhu dhidi maadui zao.

Tayari Marekani imesema ikiwa itathibitika kuwa ni yeye, wanajeshi wake watamsaka popote alipo na kuhakikisha wamemuangamiza kabisa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.