Pata taarifa kuu

Urusi: Kuna haja ya kuzuia mapigano kati ya majeshi ya Uturuki na Syria

Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan wamesisitiza kuhusu "haja ya kuzuia mapigano kati ya majeshi ya Uturuki na Syria kaskazini mwa Syria.
Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan wamesisitiza kuhusu "haja ya kuzuia mapigano kati ya majeshi ya Uturuki na Syria kaskazini mwa Syria. Sergei Ilnitsky / POOL / AFP

Urusi inasema haitakubali mapigano kutoka kati ya wanajeshi wa Syia na Uturuki. Wakati huo huo Rais wa Urusi Vladimir Putin amemwalika Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa ziara ya kiserikali jijini Moscow katika siku zijazo, wakati wa mazungumzo ya simu.

Matangazo ya kibiashara

"Vladimir Putin amemwalika Recep Tayyip Erdogan kwa ziara ya kikazi katika siku zijazo. Mwaliko umekubaliwa, " ikulu ya Kremlin imetangaza katika taarifa. Viongozi hao wawili wamesisitiza kuhusu "uwezekano wa kuzuia mapigano kati ya majeshi ya Uturuki na Syria" kaskazini mwa Syria, taarifa hiyo imongeza.

Kauli hii ya Urusi, inakuja, wakati huu vikosi vya Uturuki vikiendelea kupambana na wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini mwa Syria.

Kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo wiki iliyopita, kulitoa nafasi kwa wanajeshi wa Uturuki kuvuka mpaka na kuanza vita dhidi ya Wakurdi, kundi ambalo Utuuruki inasema ni maadui zake.

Rais Donald Trump amekuwa akitetea uamuzi wa kuondoa wanajeshi wake Kaskazini mwa Syria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.