Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-USALAMA

Vikosi vya Syria vyaingia Kobane

Mapigano makali yanashuhudiwa karibu na mji wa mpakani wa Ras al-Ain, ambapo jeshi la Uturuki na washirika wake wameshindwa kusonga mbele kutokana na upinzani kutoka wapiganaji wa Kikurdi.
Mapigano makali yanashuhudiwa karibu na mji wa mpakani wa Ras al-Ain, ambapo jeshi la Uturuki na washirika wake wameshindwa kusonga mbele kutokana na upinzani kutoka wapiganaji wa Kikurdi. REUTERS/Murad Sezer

Vikosi vya Syria vimeendelea kutumwa Kaskazini na Kaskazini-Mashariki mwa Syria, katika maeneo yanaodhibitiwa na wanamgambo wa Kikurdi, huku mapigano kati ya jeshi la Uturuki na wapiganaji wa Kikurdi yakiendelea kurindima katka maeneo hayo.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la jeshi la Syria kuingia katika mji wa Ain al-Arab lilicheleweshwa kwa muda wa siku tatu na vikosi vya umoja wa kimataifa ambavyo vilikuwa vikimalizia kuvunja kambi zao katika mkoa huo, mwandishi wetu Beirut, Paul Khalifeh, ameeeleza.

Siku ya Jumatano jioni, msafara wa magara ya jeshi la Syria ukiongozana na magari ya jeshi la Urusi yaliingia katika mji huu. Mnamo mwaka 2014 kundi la Islamic State lilipata hasara kubwa kwa mara ya kwanza katika mji wa Kobane dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi, baada ya vita iliyodumu miezi mitano.

Vikosi vyaSyria pia vinaendelea kupelekwa karibu na mji wa Tall Tamr, karibu na mpaka na Uturuki, katika mkoa wa Hassake, kaskazini mashariki mwa Syria

Vikoi vya Syria anajiandaa kuingia katika mji wa Raqqa, mji mkuu wa zamani wa kundi la Islamic State, baada ya askari wa Marekani na washirika wao kutoka nchi za Magharibi kuondoka katika mji huo.

Wakati huo huo mapigano makali yanaendeleakati ya wapiganaji wa Kikurdi na jeshi la Uturuki likisaidiwa na washirika wake, baadhi ya raia wa Syria.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.