Pata taarifa kuu
LEBANON-USALAMA-UCHUMI

Lebanon: Saad Hariri apendekeza mfululizo wa hatua kwa kumaliza mgogoro

Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri, Mei 7, 2018.
Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri, Mei 7, 2018. REUTERS/Mohamed Azakir

Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri ameendelea kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa ili kujaribu kupata uungwaji wao mkono kwa "mpango" wa kuokoa uchumi, ambao utajadiliwa Jumanne hii na Baraza la Mawaziri.

Matangazo ya kibiashara

Jitihada hizi zinafanyika wakati maandamano makubwa ya kiraia yakiingia siku yake ya nne.

Mpango huu wa kuiokoa nchi uliotayarishwa na Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri ni tofauti na sera za zamani za kiuchumi na kifedha.

Bw Hariri amependekeza bajeti ya mwaka 2020 ambayo haijumuishi kodi yoyote mpya, na nakisi inayo karibia 0%.

Badala ya kutoza kadi kwa watu wenye hali duni, ana mpango wa kuitaka sekta ya benki kuchangia kwa kiwango cha dola bilioni tatu.

Pia ameahidi kuongeza kasi mpango wa kukarabati sekta ya umeme, na kurudi kwa ugavi wa umeme saa 24 kwa siku mwaka ujao.

Waziri Mkuu amependekeza mishahara ya mawaziri, wabunge, maafisa wakuu wa serikali na mahakimu kupunguzwa.

Mpango huu, ambao pia unajumuisha hatua zingine zilizoelezwa kama za "kipekee", zimekubaliwa na vyama vikuu na unatarajiwa kujadiliwa Jumatatu hii, Oktoba 21 saa sita na Baraza la Mawaziri, ambalo linakutana kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mgogoro huo Oktoba 17.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.