Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Watano waangamia katika shambulio la kujitoa mhanga Kabul

Vikosi vya Afghanistan vikimarisha uinzi katika eneo la shambulizi, Septemba 17, 2019.
Vikosi vya Afghanistan vikimarisha uinzi katika eneo la shambulizi, Septemba 17, 2019. REUTERS/Omar Sobhani

Watu wasiopungua watano wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga magharibi mwa mji wa Kabul, shambulio lililotokea leo Jumanne asubuhi, vmamlaka imesema. Huu ni mlipuko wa kwanza baada ya miezi miwili ya utulivu katika mji mkuu wa Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

"Mapema subuhi, mshambuliaji wakujitoa mhanga, alijilipua na kuua watu watano wakiwemo raia wawili na askari watatu," Waziri wa Mambo ya Ndani Nasrat Rahimi ameliambia shirika la Habari la AFP.

Shambulio hilo pia limewajeruhi watu kumi na wawili, ikiwa ni pamoja na raia watano, amesema Rahimi, na kuongeza kuwa idadi hii inaweza kubadilika.

Wizara ya Ulinzi imesema katika taarifa kwamba watu watano wameuawa - raia mmoja na wanne kutoka vikosi vya usalama - na sita wamejeruhiwa.

Hakuna kundi ambalo limedaikuhusika na tukio hilo, ambalo lilitokea kwenye eneo la kwanza la ukaguzi kwenye lango la Chuo Kikuu cha jeshi, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vilivyoshuhudia tukio hilo na maafisa wa usalama.

Mkuu wa polisi wa Kabul amethibitisha shambulio hilo na kudai kuwa yeye ndio alikuwa amelengwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.