Pata taarifa kuu
IRAN-HAKI

Iran: Fariba Adelkhah ahukumiwa kifungo cha miaka mitano

Mtafiti Fariba Adelkhah, raia wa Ufaransa mwenye asli ya Iran, Septemba 19, 2012.
Mtafiti Fariba Adelkhah, raia wa Ufaransa mwenye asli ya Iran, Septemba 19, 2012. Thomas ARRIVE / Sciences Po / AFP

Mahakama ya nchini Iran imemhukumu mtafiti Fariba Adelkhah, raia wa Ufansa mwenye asili ya Iran kifungo cha miaka mitano, akishtumiwa "kutaka kuhatarisha usalama wa taifa", amesema mwanasheria wake.

Matangazo ya kibiashara

Mtaalam huyu, na mtafiti mwenye umri wa miaka 61, ameendelea kusema kuwa hana hatia.

Hatua ya kukamatwa kwake mnamo mwezi Juni 2019, kama alivyokamatwa mtafiti mwingine kutoka Ufaransa Roland Marchal - aliyeachiliwa hivi karibuni - ilikosolewa na serikali ya Ufaransa, ambayo anaomba aachiliwe huru.

Mtafiti huyo amehukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa "kukutaka kuhatarisha usalama wa taifa" na kifungo cha mwaka mmoja kwa "propaganda dhidi ya mfumo wa kisiasa" wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini latatumikia adhabu ya muda mrefu, amesema wakili Saïd Dehghan.

Hata hivyo wakaili wake amesema kuwa licha ya hukumu hiyo watakata rufaa.

Kesi ya Fariba Adelkhah ilifunguliwa Machi 3 mbele ya kitengo cha 15 cha Mahakama ya Mapinduzi ya Tehran.

Baada ya kusikilizwa kwa mara ya pili Aprili 19, wakili wake alisema ana imani ya mteja wake kuachiliwa huru. Siku chache baada ya kuzuiliwa Fariba Adelkhah alifanya mgomo njaa wa siku 49 kati ya mwishoni mwa mwezi wa Desemba na Februari, kulingana na Dehghan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.