Pata taarifa kuu
GABON-GINE YA IKWETA

Ghana na Mali nazo zafuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya AFCON 2012

Emmanuel Badu wa timu ya Ghana akishangilia goli alilofunga dhidi ya Guinea
Emmanuel Badu wa timu ya Ghana akishangilia goli alilofunga dhidi ya Guinea Reuters

Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika imeendelea hapo jana kwa kushuhudia mechi za mwisho za makundi na hatimaye sasa timu zitakazocheza hatua ya robo fainali ya mwaka huu zimekwishajulikana na mitanange hiyo itaanza kupigwa tarehe 4 ya mwezi huu.

Matangazo ya kibiashara

Katika mechi za jana jioni timu ya taifa ya Botswana wenyewe walikuwa wenyeji wa timu ya taifa ya Mali, kwenye mchezo ambao umeshuhudia timu ya Mali ikifuzu hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Botswana kwa jumla ya mabo 2-1.

Magoli ya mali yalifungwa na Garra Dembele na Seydou Keita wakati lile goli la kufutia machozi la timu ya taifa ya Botswana likifungwa na Mogakolodi Ngele.

Mchezo mwingine uliopigwa hapo jana jioni uliwakutanisha timu ya taifa ya Ghana ambao walikuwa wakicheza na timu ya taifa ya Guinea kwenye mchezo ambao umeshuhudia timu hizo zikitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Kwa matokeo hayo sasa timu nane zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali ambazo ni, Ghana, Tunisi, Mali, Gine ya Ikweta, Gabon, Sudan, Cote d'Ivoire pamoja na zambia.

Mechi za robo fainali zitaanza kuchezwa tarehe 4 ya mwezi huu ambapo mchezo wa awali utawakutanisha timu ya Zambia ambayo itacheza na Sudan, wakati katika mchezo wa pili Cote d'Ivoire itapambana na wenyeji Gine ya Ikweta.

Tarehe 5 yani siku inayofuata mechi nyingine za robo fainali zitachezwa ambapo timu ya taifa ya Gabon ambao ni wenyeji wengine watacheza na Mali wakati Ghana watakuwa wenyeji wa Tunisia.

Nusu fainali ya michuano hiyo itapigwa tarehe 8ya mwezi huu ambapo leo na kesho ni mapumziko.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.