Pata taarifa kuu
JAMAICA

Usain Bolt ajigamba kuvunja rekodi zake za mita 100 na 200 kwenye mashindano ya Olympic 2012 London

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 100 na 200 Usain Bolt
Bingwa wa dunia wa mbio za mita 100 na 200 Usain Bolt Reuters

Bingwa mara tatu wa mashindano ya Olympic, Mjamaika Usain Bolt amejigamba kuvunja rekodi yake mwenye aliyoiweka kwenye mashindano ya dunia yaliyopita. 

Matangazo ya kibiashara

Mfukuza upepo huyo amesema kuwa kwenye Olypic ya mwaka huu anataka kuvunja rekodi yake ya mbio za mita 100 ambapo alitumia muda wa sekunde 9.58 na sasa anajinasibu kuweka rekodi ya sekunde 9.4.

Nguli huyo ameendelea kutamba kuwa katika mbo za mita 200 anataka kuvunja rekodi yake ya awali ya sekunde 19.19 na kwamba anataka kuweka rekodi ya sekunde 19 pekee.

Akizungumzia ushindi wake wa Medali tatu za dhahabu kwenye Olympic ya mwaka 2008, Bolt amesema kuwa kwasasa anataka kuushangaza ulimwengu kwa kile atakachokifanya kwenye mashindano ya mwaka huu.

Mashindano ya Olympic ya London yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 27 ya mwezi huu ambapo zimebaki siku 100 pekee.

Kwa upande wa waogeleaji, bingwa mara 14 wa mchezo huo rais wa Marekani Michael Philips amesema anatarajia kufanya makubwa kwenye michuano ya mwaka huu na kwamba pia anataka kuweka rekodi mpya ya kuogelea.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.