Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha wa Newcastle United Pardew akiri Demba Ba huenda akaondoka January mwakani

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal anayekipiga katika Klabu ya Newcastle United Demba Ba
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Senegal anayekipiga katika Klabu ya Newcastle United Demba Ba

Kocha Mkuu wa Newcastle Alan Pardew amekiri mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal na mfungaji bora wa timu hiyo msimu uliopita Demba Da huenda akaondoka mwezi January kwa kitita cha pauni milioni saba. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na saba amekiri kutokuwa na raha kutokana na kutokuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha Newcastle United katika msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Pardew amesema kulingana na kifungu ambacho kipo kwenye mkataba wa Demba Ba kinatoa nafasi kwa mshambuliaji huyo kuondoka mwishoni mwa mwezi january kama mambo yataenda tofauti.

Demba Ba ambaye alifunga magoli kumi na tisa katika msimu uliopita amekuwa akichukizwa na kitendo cha kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza na kuwa mshambuliaji kiongozi nafasi ambayo ameichukua Pappiss Demba Cisse.

Demba Ba ambaye hajajumuisha kwenye kikosi cha Newcastle ambacho kimesafiri kuelekea nchini Ureno kwa ajili ya mashindano ya EUROPA dhidi ya Maritimo amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa za Uingereza.

Kabla ya Pardew kutoa kauli hii mapema jumatatu alinukuliwa akisema Demba Ba na yeye hawana tofauti zozote ambazo zimechangia kuwekwa benchi katika mechi kadhaa za msimu huu.

Demba Ba aliingia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Everton na kuisaidia kupata sare ya magoli 2-2 huku magoli yote akifunga mwenyewe na kuonekana wembe mkali ukilinganisha na washambuliaji waliotanguliwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.