Pata taarifa kuu
SOKA-UINGEREZA

Daniel Sturridge apongezwa kwa kuipaisha Liverpool katika mechi yake dhidi ya Everton

http://thefootballspace.com

Kocha wa klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza, Brendan Rodgers amempongeza mshambuliaji Daniel Sturridge aliyetokea benchi na kuingia dimbani katika dakika 11 za mwisho kabla ya kupachika bao lililosawazisha mechi hiyo na kufanya sare ya goli 3-3 dhidi ya Everton jana jumamosi katika dimba la Goodison Park.

Matangazo ya kibiashara

Sturridge aliingia dimbani katika dakika za lala salama na kufifisha matumaini ya Everton kutwaa ushindi wa pili katika mechi za mahasimu wa jiji, na hilo ni bao la 11 kwa Sturridge katika msimu huu.

Mabao mengine ya Liverpool yalipachikwa na Philippe Coutinho katika dakika ya 5 na Luis Suarez katika dakika ya 19 ya mchezo huo.

Katika kipindi cha pili Everton ndio waliokuwa mbele kwa bao 3 mpaka Sturridge aliposawazisha katika dakika ya 89 ya mchezo huo.

Kwa matokeo hayo Liverpool wako katika nafasi ya 2 baada ya kushinda mechi 7, na wana pointi 3 mbele ya Everton walio katika nafasi ya 6 baada ya kushinda mechi 5 pekee.

Arsenal nayo imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi msimu huu baada ya kujipatia pointi 4 zaidi kupitia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton, hivi sasa inaongoza msimamo ikiwa na pointi 28, mbele ya Liverpool yenye pointi 24 sawa na Chelsea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.