Pata taarifa kuu
SOKA

Everton yaiacha kinywa wazi Manchester United kwa bao 1-0

Manchester wakivaana na Everton
Manchester wakivaana na Everton Telegraph.co.uk

Klabu ya soka ya Uingereza Manchester United imeendelea kupata matokeo mabaya katika ligi kuu ya soka nchini humo baada ya kufungwa bao 1 kwa 0 na Everton jana usiku.

Matangazo ya kibiashara

Bao la Bryan Oviedo dakika nne kabla ya kumalizika kwa mchuano huo ulipeleka kilio kwa mashabiki wa Manchester United huku Everton ikimaliza ukame wa miaka 21 kwa kuifunga Manchester United katika uwanja wake wa nyumbani wa OLD TRAFFORD.

Juhudi za washambulizi wa Manchester United kama Wayne Rooney na Danny Welbeck kuitafutia klabu yao ushindi ziliambulia patupu kutokana na mashambulizi yao kugonga mwamba mara kadhaa wakati Manchester United ikikosa huduma za mshambuliaji Robin Van Persie ambaye anauguza jeraha.

Kocha wa United David Moyes ambaye pia wakati mmoja alikuwa kocha wa Everton amesema kuwa amesikitishwa mno na matokeo ya jana ambayo yanaiweka timu yake katika nafasi ya 9 ikiwa na alama 22 katika msururu wa ligi kuu.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.