Pata taarifa kuu
RIADHA

Usain Bolt atajwa kuwa mwanariadha bora wa Jamaica kwa mwaka 2013

Mwanaraiadha wa Jamaica  Usain Bolt,
Mwanaraiadha wa Jamaica Usain Bolt, REUTERS/Dylan Martinez

Mabingwa mara mbili wa medali za dhahabu katika mashindano ya dunia ya mbio fupi Usain Bolt na Shelly-Ann Fraser-Pryce jana Jumatatu wametajwa na chama cha wanariadha nchini Jamaika kuwa wanariadha bora wa Jamaika kwa mwaka 2013, Bolt kwa upande wa wanaume na Shelly-Ann kwa upande wa wanawake. 

Matangazo ya kibiashara

Bolt amekuwa nje ya nchi yake kutokana na majukumu ya ufadhili na Fraser-Pryce, walirejesha ubingwa walioshinda mwaka jana.

Bolt alishinda mita 100,na mita 200 mara mbili katika mashindano ya dunia ya IAAF jijini Moscow Mapema mwaka huu, na kuongoza timu ya relay ya mita 400 kupata ushindi.

Fraser-Pryce Pia alishinda mara mbili mbio za miata 100m na 200m.

Mapema mwaka huu Bolt na Fraser-Pryce walitajwa na IAAF kuwa wanariadha bora wa mwaka katika hafla iliyofanyika mjini Monaco na wanatazamiwa kushinda tuzo ya wanamichezo bora wa kike na wa kiume nchini Jamaika baadaye mwakani
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.