Pata taarifa kuu
LIGI KUU UFARANSA-PSG-LYON-Soka

Nyota wa PSG aendelea kuuguza jeraha la kisigino

Zlatan Ibrahimovic akikabiliana na mchezaji wa klabu ya Lyon Jordan Ferri kwenye uwanja wa Parc des Princes, Septemba 21 mwaka 2014.
Zlatan Ibrahimovic akikabiliana na mchezaji wa klabu ya Lyon Jordan Ferri kwenye uwanja wa Parc des Princes, Septemba 21 mwaka 2014. THOMAS SAMSON / AFP

Mchezaji nyota wa Paris Saint Germain, Zlatan Ibrahimovic, hajashiriki kwa majuma kadhaa michuano ya ligi kuu ya Ufaransa kutokana na jeraha la kisigino. Mchezaji huyo ameitishwa na Uswisi.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivo daktari anaye muhudumia, Leif Sward, amepuuzia wito huo akisema haitowezekana Ibrahimovic ashirikishwe katika mechi hata moja wakati bado anaendelea kusumbuliwa kwenye kisigino, licha ya kuwa hakuna uvimbe.

“ Tumeanziosha vipimo vya kitabibu , lakini naendelea kushangazwa na jeraha hilo, kwani hakuna uvimbe, na hilo ndio linanitia wasi wasi” amesema Leif Sward.

“Ni wiki kadhaa sasa tangu Ibrahimovic apate maumi hayo, lakini hatujui yanatokana na nini”, ameendelea kusema Sward.

Kwa upande wake Ibrahimovic ameonekana kutii amri ya daktari wake, na kuelezea masikitiko yake kuona alicheza mechi iliyoikutanisha klabu yake na Lyon siku 15 zilizopita, wakati alikua bado hajapona jeraha.

“ Nilitaka kwenda haraka, wakati nilitakiwa nipumzike”, amesema Ibrahimovic katika mkutano na waandishi wa habari, huku akibaini kwamba alitakiwa apumzikishe muili wake wakati anauguza jeraha la kisigino. Haijajulikana iwapo nyota huyo wa PSG atacheza wakati klabu yake itamenyana na Urusi Ijumaa wiki hii.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.