Pata taarifa kuu
USAJILI-ULAYA

Liverpool yamnasa beki wa kushoto wa Southampton, Nathaniel Clyne, Beyern yamnasa Douglas Costa

Mchezaji mpya wa Liverpool, Nathaniel Clyne anayejiunga na klabu hiyo akitokea Southampton
Mchezaji mpya wa Liverpool, Nathaniel Clyne anayejiunga na klabu hiyo akitokea Southampton liverpoolfc.com

Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza hatimaye imefanikiwa kupata saini ya beki wa kushoto wa klabu ya Southampton, Nathaniel Clyne, huku mabingwa wa Ujerumani Beyern Munich wakifanikiwa kupata saini ya kiungo wa Brazili, Douglas Costa kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine.  

Matangazo ya kibiashara

Liverpool imefanikiwa kumnasa beki huyu wa kimataifa wa Uingereza baada ya dau lao la awali ya paundi milioni 10 kukataliwa na klabu ya Southampton, ambapo sasa mchezaji huyo amekubalia mkataba wa miaka mitano na vijogoo wa jiji kwa dau la paundi milioni 12.

Akinukuliwa kwenye mtandao wa klabu ya Liverpool mara baada ya kutia saini mkataba wake, Clyne anasema kuwa amefutahi na ni kama ndoto yake imekuwa kweli kujiunga na klabu kubwa kama Liverpool na yenye historia katika soka la barani Ulaya.

Clyne ameongeza kuwa mapema tu wakati Liverpool ilipoonesha nia ya kutaka kumsajili, alikuwa tayari na wakati wote alitamani timu yake ifikie makubaliano na kuweza kumsajili jambo ambalo limetimia.

Clyne ambaye alikuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na klabu ya Southampton anakuwa mchezaji wa 6 kusainiwa na klabu hiyo.

Nchini Ujerumani, mabingwa wa Bundesliga klabu ya Bayern Munich yenyewe imetangaza kufanikiwa kumnasa kiungo wa kibrazili, Douglas Costa kutoka klabu ya Shakhtar ya UKraine kwa dau la paundi milioni 21.

Mchezaji mpya wa Bayern Munich, Douglas Costa
Mchezaji mpya wa Bayern Munich, Douglas Costa Reuters

Costa mwenyewe baada ya kutia saini mkataba wake, amesema kuwa ndoto zake zimetimia kwa kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Ulaya.

Usajili wa Costa unazidisha uvumi kuwa umetokana na ukweli kuwa huenda kiungo wake Bastian Schwensteiger akajiunga na klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza.

Kocha wa Bayern, Pep Guardiola sasa anao wigo mpana wa kuchagua viungo kwenye timu yake kwakuwa tayari anao wachezaji kama, Mfaransa, Franck Ribery, muhispania Thiago Alcantara, Xabi Alonso na Javi Martinez.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.