Pata taarifa kuu
MISRI-ZAMALEK FC-SOKA

Zamalek FC yajiondoa katika Ligi kuu ya soka

Zamalek, mshindi wa Kombe la Misri, yajiondoa katika Ligi kuu nchini Misri.
Zamalek, mshindi wa Kombe la Misri, yajiondoa katika Ligi kuu nchini Misri. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

Klabu ya soka ya Zamalek FC kutoka nchini Misri, imetangaza kujiondoa katika ligi kuu ya soka nchini humo kwa madai ya kuonewa na refarii.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa klabu hii umekuja baada ya kufungwa na klabu ya Tala'ea El-Gaish mabao 3 kwa 2 katika mchuano wa ligi kuu mwishoni mwa juma lililopita.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini humo, wamesema hatua ya refarii wa kati ya kumpa kadi nyekundu beki wao Ali Gabr na kuipa Tala'ea mkwaju wa penalti ilikuwa ni makosa.

Kabla ya mchuano huo, uongozi wa klabu hiyo ulisema ulikuwa umemlalamikia mwamuzi wa kati aliyechezesha mchuano huo Mahmoud al-Banna.

“Inaonekana, kulikuwa na lengo la kumkabidhi na kumteua Banna katika mchuano huu ili kuionea Zamalek”, taarifa ya Zamalek imeeleza.

Zamalek imejiondoa katika ligi hiyo huku ratiba ya ligi kuu nchini humo ikitarajiwa kuwa dhidi ya Ghazl El Mahalla siku ya Jumatano wiki hii.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.