Pata taarifa kuu
MONACO-NANTES-SOKA

Ligi kuu: Monaco yatoka sare dhidi ya Nantes

Ocampos akiifungia klabu yake ya Monaco dhidi ya Bayer Luverkusen.
Ocampos akiifungia klabu yake ya Monaco dhidi ya Bayer Luverkusen. REUTERS/Ina Fassbender

AS Monaco, ambao wameshindwa kufanya vizuri dhidi ya Nantes wametoka sare ya kutofungana (0-0), Jumapili hii Februari 28. Matokeo hayo yanapelekea Paris-Saint-Germain (PSG) kupata ushindi wa haraka wiki ijayo kama itacheza vizuri.

Matangazo ya kibiashara

Kama PSG watapata ushindi Jumapili hii usiku dhidi ya Olympique Lyonnais (OL), kwa siku ya ishirini na nane ya michuano ya Ligi kuu, na kupata ushindi mwishoni mwa wiki ijayo wakati ambapo Monaco wameshindwa kufanya vizuri, watakuwa mabingwa wa Ufaransa.

Kwa sasa, Monaco na Nanteswamefanya vizuri kwa kugawana pointi hizi. Monaco, ambayo ni ya pili, ina pointi tisa mbele ya Nice, Rennes na Saint-Etienne.

Nantes hawajafungwa katika mechi kumi na sita

Nantes mpaka sasa hawajafungwa katika mechi kumi na sita katika mashindano yote, na pia wajafungwa katika mechi kumi na tatu katika michuano ya Ligi kuu. Nantes, ambayo inachukua nafasi ya sita, iko katika timu ambazo zinapewa nafasi ya kufanya vizuri, ikusubiri mechi ya klabu ya Kijani. Wachezaji wa Michel Der Zakarian wanapania kupata hata mechi moja, kwani wangelipaswa kucheza dhidi ya Bastia lakini mechi hii iliahirishwa wiki mbili zilizopita.

Jumapili hii usiku, macho yote yatakua yameelekezwa kwa klabu ya Lyon, itakayoipokea PSG ambayo tayari imeifunga mara nne msimu huu katika mashindano yote. Marco Verratti na Angel Di Maria, wanakabiliwa na matatizo ya kimwili, hawatocheza katika safu ya PSG. Lakini OL watakua na kibarua kigumu katika mechi hii, baada ya kutokuwepo kwa Mathieu Valbuena, Corentin Tolisso Clement Grenier, Christophe Jallet na Samuel Umtiti.

Mechi ya Ajaccio-Marseille, iliopangwa kuchezwa Jumapili saa 11 jioni, imeahirishwa kutokana na hali mbaya ya uwanja baada ya siku mbili za mvua na utabiri wa hali mbaya ya hewa ikiendelea.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.