Pata taarifa kuu
MAN CITY-PSG-UEFA

Ligi ya Mabingwa: Manchester City yawaangusha PSG

Mbelgiji wa Manchester City, Kevin De Bruyne (kushoto), akikabiliana na beki wa PSG, Marquinhos.
Mbelgiji wa Manchester City, Kevin De Bruyne (kushoto), akikabiliana na beki wa PSG, Marquinhos. Reuters / Darren Staples

Paris Saint-Germain imeondolewa kwa mwaka wa nne mfululizo katika robo fainali ya soka ya michuano ya Ligi ya MabingwaJumanne, Aprili 12, 2016. PSG imefungwa na Manchester City 1-0 katika mechi ya marudiano baada ya kutoka sare ya kufungana 2-2 katika mechi ya awali.

Matangazo ya kibiashara

Kwa hiyo Manchester city imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya ushindi huo dhidi ya PSG.

Manchester City wamepata ushindi huo wakiwa nyumbani katika uwanja wa Etihad. Bao hilo la Manchester city limewekwa wavuni katika dakika ya 76 kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji De Bruyne.

Kwa ushindi huo Manchester city wameifunga Psg jumla ya mabao 3-2 baada ya timu hizo kufungana bao 2-2 katika mchezo wa awali.

Mechi nyingine iliyopigwa Jumanne hii ni kati ya Real Madrid na Wolf-Sburg. Real Madrid imepata ushindi wa mabao 3-0. Maboa yote hayo yalifungwa na mchezaji Christiano Rolnado.

Katika mchezo wa awali Wolf-Sburg waliwashinda Real Madrid mabao 2-0, Kwa sasa Real Madrid wameingia katika hatua ya Nusu fainali.

Jumatano hii kutachezwa mechi mbili. Atletico Madrid Benfica itajitupa uwanjani kumenyana na Barcelona. Nao Benfica watamenyana na Bayern Munich.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.