Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO-FIFA-RUSHWA

Blatter: "niliombwa na Uswisi kuingilia katika mgogoro wa Burundi"

Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter akipongezwa kwa noti za Dola, Julai 20, 2015 katika Zurich
Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter akipongezwa kwa noti za Dola, Julai 20, 2015 katika Zurich AFP

Sepp Blatter, rais wa zamani wa FIFA amesema Alhamisi hii kuwa alitumwa mwezi Mei 2015 na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi, kwa ombi la Marekani kumshawishi Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, asiwezi kuwania katika uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

"Uswisi, ambayo ilitaka kutetea maslahi ya Burundi, iliniomba kuzungumza na Rais Pierre Nkurunziza, ambaye pia ni shabiki mkubwa wa mpira wa miguu, ili kumshawishi asiwezi kugombea muhula wa tatu," Sepp Blatter amesema kwa yombo vya habari baada ya kuwasilisha mjini Zurich wasifu wake ambapo alifichua jukumu hilo la kidiplomasia alilopewa ambalo lilikua bado siri.

Amesema katika kitabu hicho kwamba kazi hiyo ya kumshawishi Rais Nkurunziza kwa niaba ya Uswisi ilifanyika "kwa ombi la Marekani" ili kujaribu kutatua mgogoro wa Burundi.

"Tulimpendekeza Nkurunziza kuwa balozi wa soka barani Afrika au nje ya Afrika. Rais Nkurunziza alisema nimeguswa na ombi hilo, nami nitakupa jibu. Nilimuomba nikisisitiza, hatimaye alifikiria na baada ya muda, alijibu, hapana kwa kweli ntawania katika uchaguzi wa urais, " Blatter ameongeza.

Amesema kuwa mkutano huo ulifanyika mwezi Mei, kabla ya kuzuka kwa kashfa ya rushwa katika Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA). "Hii si mara ya kwanza kufanya jambo kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi," ameongeza rais wa zamani FIFA. "Nilimualika au nilimtaarifu Balozi au afisa mwandamizi katika Wizara ya mambo ya Nje ya Uswisi kuhusu ziara yangu. Wakati mwingine aliweza hata kuhudhuria mkutano na rais wa jamhuri na hakuweza kufanya hivyo mwenyewe, kwa sababu soka inafungua milango kwa wote".

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi (FDFA) "imethibitisha kuwa kulikuwa na mawasiliano kati ya Katibu Dola Yves Rossier na Bw Joseph Blatter. Nia ilikuwa kuchangia katika ufumbuzi wa amani kwa kutatua mgogoro wa sasa nchini Burundi. " Lakini "FDFA haijawahi kumuomba rais Nkurunziza kutowania katika uchaguzi wa rais," Wizara ya mambo ya Nje ya Uswisi imeongeza.

Burundi imetumbukia katika mgogoro mkubwa tangu Bw Nkurunziza kutangaza mwezi Aprili 2015 nia yake ya kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi Julai mwaka jana, uchaguzi ambao mpaka sasa upinzani, mashirika ya kiraia na jumuiya ya kimataifa hawautambui. Machafuko nchini Burundi yamesababisha zaidi ya vifo vya watu 500 na watu zaidi ya 270,000 kulazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.