Pata taarifa kuu
UEFA-SOKA

Sevilla na Villarreal zajipatia nafasi nzuri

Liverpool yaangukia pua kwa kufungwa ugenini dhidi ya Villarreal bao 1-0, Alhamisi Aprili 28, 2016.
Liverpool yaangukia pua kwa kufungwa ugenini dhidi ya Villarreal bao 1-0, Alhamisi Aprili 28, 2016. (Photo : Reuters)

Klabu za Uhispania zinaonekana kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Ulaya (Europa League). Katika mechi za kwanza za nusu fainali zilizopigwa Alhamisi hii kati ya Sevilla na Donetsk, klabu hizi zimelazimika kwenda sare ya kufungana mabao 2-2, wakati ambapo Sevilla imekua ikichezea ugenini.

Matangazo ya kibiashara

Mechi nyingine iliyopigwa jana ilizikutanisha timu za Villarreal na Liverpool, ambapo Liverpool ilikubali kusalimu amri kwa kufungwa bao 1-0.

Shakhtar Donetsk-Sevilla

Sevilla, mabingwa watetezi mara mbili, wamepiga hatua nzuri dhidi ya Shakhtar Donetsk, kwa kufunga mabao mawili ugenini, kupitia Vitolo katika dakika ya 6 ya mchezo na mchezaji kutoka Ufaransa Kevin Gameiro, ambaye aliifungia klabu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 82 (2-2) .

Mchuano huo uliochezwa katika uwanja wa Arena de Lviv, Magharibi mwa nchi, ulikua mzuri tena wa kufurahisha. Bao la kwanza la kusawazisha kwa klabu ya Shakhtar Donetsk lilifungwa na Marlos (1-1) katika dakika ya 23 kabla ya Stepanenko kufunga bao la pili katika dakika ya 36.

Lakini Sevilla, pia mshindi mwaka 2006 na 2007, ambao wamemaliza vizuri katika mchuano huo wa kwanza wa nusu fainali na wana bahati ya kufuzu katika mchuano wa marudiano ambao utachezwa nyumbani Mei 5 katika uwanja wa Andalusia. Hata hivyo Shakhtar Donetsk bado wana matumaini ya kufanya vizuri ugenini.

Villarreal-Liverpool

Bao lililofungwa katika muda wa nyongeza lilipelekea Villarreal kuiangusha Liverpool (1-0), na kuipa klabu hiyo ya Hispania nafasi nzuri ya kufuzu kwa mechi ya marudiano itakayochezwa ndani ya wiki moja.

Katika sekunde ya mwisho kabisa katika uwanja wa Madrigal, Adrian Lopez alipata fursa ya kutumbukiza mpira katika wavu wa Liverpool, na hivyo kuandikisha bao la ushindi katika dakika ya (90+2).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.