Pata taarifa kuu
SOKA-PSG-SERGE AURIER

Aurier ahukumiwa kifungo cha miezi 2 jela

Licha ya hukumu dhidi yake, Serge Aurier anaweza akacheza Jumatano hii dhidi ya Ludogorets Razgrad ya Bulgaria.
Licha ya hukumu dhidi yake, Serge Aurier anaweza akacheza Jumatano hii dhidi ya Ludogorets Razgrad ya Bulgaria. Getty Images

Beki wa PSG kutoka Côte d’Ivoire, Serge Aurier, amehukumiwa Jumatatu hii Septemba 26 kifungo cha miezi miwili jela kwa vurugu alizofanya kwa hiari kwa wa serikali. Mahakama ya mjini Paris pia imemuhukumu Serge Aurier kulipa Euro 600 kwa uharibifu.

Matangazo ya kibiashara

Ametakiwa pia kulipa Euro 1,500 katika gharama za mahakama.

mchezaji huyo wa soka mwenye umri wa miaka 23 alifanya mabishano na askari polisi alipokua akitokea katika sehemu za starehe mjiniParis mwezi Mei.

Hukumu dhidi ya mchezaji wa kimataifa haitomkataza kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Jumatano, 28 Septemba, dhidi ya klabu ya Bulgaria ya Ludogorets Razgrad.

Hata hivyo Bw Aurier amekataa rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya mjini Paris.

Aurier alifanya madhambi ya aina yake Ijumaa, 23 Septemba, wakati mechi kati ya PSG dhidi ya Toulouse, mchuano ambao mchezaji huyo alilazimika kufukuzwa. Katika mchunao huo PSG iliibuka mshindi kwa kufunga mabao 2-0

Wakati wa msimu uliopita, Serge Aurier alitoa maeneo katika video, maneno yaliyotajwa kuwa ni matusi dhidi ya Laurent Blanc, Kocha wa PSG. Aurier pia alimwita mchezaji Angel Di Maria kuwa ni "Clown" yaani mpumbavu, katika maoni aliotoa na kurushwa katika mitandao ya kijamii.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.