Pata taarifa kuu
LIVERPOOL-SOKA

Sadio Mané achaguliwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Uingereza

Sadio Mane wa Liverpool aliynunuliwa pesa nyingi katika historia ya mchezaji wa kiafrika.
Sadio Mane wa Liverpool aliynunuliwa pesa nyingi katika historia ya mchezaji wa kiafrika. © Getty Images

Mshambuliaji wa Senegal Sadio Mané, kutoka klabu ya Liverpool, amechaguliwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Uingereza kwa kipindi cha miezi ya Agosti na Septemba.

Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kura ya mashabiki, Mané anaongoza dhidi ya mchezaji kutoka Ubelgiji Kevin De Bruyne, anayeichezea Manchester City, na Mfaransa Etienne Capoue anayeichezea klabu ya Watford. Kevin De Bruyne amechukua nafasi ya pili, naye Etienne Capoue amechukua nafasi ya tatu.

Sadio Mané, mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao matatu katika michezo ya kwanza sita ya Ligi Kuu 2016-2017.

Sadio Mané alitoa pasi tatu nzuri.

Mhispania mwenye asili ya Brazil Diego Costa anayeichezea Chelsea, wachezaji wa Uingereza Michail Antonio anayeichezea West Ham na Curtis Davies, anayeichezea Hull City walikuwa wameshindia nafasi hii.

Liverpool klabu ya mshambuliaji huu wa Senegal, sasa inachukua nafasi ya nne katika Ligi Kuu.

Liverpool ilitoa kitita cha Euro milioni 41.2 katika soko la usajili la kumhamisha Sadio Mané kutoka Southampton kwenda klabu hiyo, jambo ambalo linamfanya mshambuliaji wa Senegal kuwa mchezaji kutoka bara la Afrika aliyenunuliwa pesa nyingi katika historia.

Mapema mwezi Septemba, alichaguliwa mchezaji bora wa Liverpool kwa kipindi cha mwezi wa Agosti.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.