Pata taarifa kuu
LIVERPOOL-SOKA

Jeraha huenda likamweka nje Sadio Mane kwa muda mrefu

Sadio Mané na mchezaji mwenzake akisherekea bao   katika mchuano dhidi ya  Tottenham tarehe 11 mwezi Februari mwaka 2017
Sadio Mané na mchezaji mwenzake akisherekea bao katika mchuano dhidi ya Tottenham tarehe 11 mwezi Februari mwaka 2017 Carl Recine / Reuters

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool nchini Uingereza Sadio Mane ambaye ni mchezaji wa Kimataifa kutoka Senegal, atakosa mchuano muhimu dhidi ya Bournemouth, siku ya Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Kocha Jurgen Klopp amesema huenda mchezaji huyo akawa nje ya uwanja hadi kumalizika kwa msimu huu.

Mane mwenye umri wa miaka 24, mwishoni mwa wiki iliyopita, alipata jeraha la goti wakati klabu yake ilipokuwa inacheza na Everton na kuisaidia kupata ushindi wa mabao 3-1.

Ripoti zinasema kuwa mchezaji huyo amevimba goti na sasa anasubiri ripoti ya mwisho kutoka kwa Daktari wake.

Hata hivyo, kocha Klopp anatarajiwa kumtumia Daniel Sturridge katika mchuano wa Jumatano lakini pia katika mechi zingine ikiwa Mane hatakuwa amepata nafuu.

Mchezaji mwingine wa Liverpool ambaye yupo nje ya uwanja kwa sababu ya jeraha ni kiungo wa kati Adam Lallana.

Lallana amekuwa nje kwa muda wa mwezi mmoja sasa kwa sababu ya jeraha la paja.

Liverpool inashikilia nafasi ya tatu katika msururu wa ligi kuu kwa alama 59.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.