Pata taarifa kuu
CHELSEA-SOKA

Conte asema Chelsea inahitaji kushinda mechi sita ili kunyakua ligi kuu

Kocha wa Chelsea  Antonio Conte akisherehekea mmoja ya ushindi katika michuano ya ligi kuu nchini Uingereza
Kocha wa Chelsea Antonio Conte akisherehekea mmoja ya ushindi katika michuano ya ligi kuu nchini Uingereza Reuters / Toby Melville Livepic

Kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte anasema wachezaji wake wanahitaji kushinda mechi sita kati ya michuano nane inayosalia ili kushinda ligi kuu nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Chelsea  wanaongoza ligi kwa alama 72 baada ya mechi 30 mbele ya Tottenham Hotspurs ambayo ina alama 62.

Siku ya Jumatano, The Blues walipata ushindi muhimu dhidi ya Manchester City kwa kuwafunga mabao 2-1.

Conte ameeleza kuwa Tottenham inaweza kushinda taji la msimu huu na hivyo wanahitaji alama 18 kujihakikishia taji hilo.

Tottenham hawajawahi kushinda ligi nchini Uingereza tangu mwaka 1961.

Ratiba kamili ya Chelsea zinazosalia:-

  • Bournemouth vs Chelsea -April 8 2017
  • Manchester United vs Chelsea -April 16 2017
  • Southampton vs Chelsea -Aprili 25 2017
  • Everton vs Chelsea -Aprili 30 2017
  • Middlebrough vs Chelsea -Mei 8 2017
  • West Brom vs Chelsea -Mei 13 2017
  • Sunderland vs Chelsea   -Mei 21 2017
  • Watford vs Chelslea -Tarehe haijapangwa
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.