Pata taarifa kuu
CAF-TP Mazembe

TP Mazembe yafanikiwa kufuzu hatua ya makundi michuano ya Shirikisho

TP Mazembe waliposhinda taji la mwaka 2016
TP Mazembe waliposhinda taji la mwaka 2016 STRINGER / AFP

TP Mazembe ya DRC ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Shirikisho barani Afrika wamefanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi baada ya mchuano wake wa mwishoni mwa juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria, imefuzu kwa sababu ya ushindi wa mabao 2-0 katika mchuano wa kwanza wiki mbili zilizopita jijini Lubumbashi.

Haya ni matokeo mazuri kwa Mazembe ambao wanataka kutetea taji hili baada ya kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Klabu hii yenye makao yake mjini Lubumbashi pia imekuwa ikabiliwa na changamoto ya kuwa kocha baada ya kocha kutoka Ufaransa Thierry Froger kufutwa kazi mwezi Machi.

Mbali na TP Mazembe, vlabu vingine ambavyo vimefuzu katika hatua ya makundi ni pamoja na:-

 

 • MC Alger-Algeria
 • Recreativo do Libolo-Angola
 • Smouha-Misri
 • CF Mounana-Gabon
 • Horoya-Guinea
 • FUS Rabat-Rabat
 • Platinum Stars-Afrika Kusini
 • SuperSport United-Afrika Kusini
 • Al-Hilal -Sudan
 • Mbabane Swallows-Swaziland
 • Club Africain-Tunisia
 • CS Sfaxien-Tunisia
 • KCCA-Uganda
 • ZESCO United-Zambia

Klabu moja inasubiriwa kati ya Rivers Unites ya Nigeria na Rayon Sport ya Rwanda.

Mchuano wa kwanza, Rivers walishinda  mabao 2-0 huku mchuano wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi jijini Kigali.

Droo ya hatua ya makundi, itafanyika tarehe 26.

Kutakuwa na makundi manne, kila kundi na timu nne.

Mshindi na yule wa pili, wote watafuzu katika hatua ya robo fainali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.