Pata taarifa kuu
CHELSEA-SOKA

Conte atia saini mkataba wa miaka 2 kuendelea kuifunza Chelsea

Kocha wa Chelsea Antonio Conte.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte. video.skysports.com

Kocha wa klabu ya Chelsea Antonio Conte ametia saini mkataba mpya wa miaka miwili.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inampa uhakika wa kuendelea kuwaongoza mabingwa hao watetezi wakati wa msimu mpya utakapoanza mwezi Agosti.

Raia huyo wa Italia amesema amefurahi kutia saini mkataba huo mpya baada ya kufanya hivyo ule wa miaka mitatu aipoingia katika klabu hiyo mwaka 2016.

Conte amesema mwaka wa kwanza katika klabu hiyo alifanya bidii yeye na wachezaji wake na mkataba huu unampa nguvu na kuendelea kufanya hivyo ili kutetea taji lao.

Kocha huyo amepewa mkataba huo baada ya mwezi Mei kunukuliwa akisema kuwa angependa kuendelea kuifunza Chelsea kwa muda mrefu.

Msimu ulipita, aliiongoza Chelsea kushinda mechi 30, na kucheza mechi 13 bila kufungwa.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.