Pata taarifa kuu
SOKA

Barcelona yaifunga Manchester United bao 1-0 mechi ya kirafiki

Wachezaji wa klabu ya Barcelona baada ya kuishinda Manchester United
Wachezaji wa klabu ya Barcelona baada ya kuishinda Manchester United Dhaka Tribune

Klabu ya Manchester United inamalizia maandalizi ya michuano yake ya kimataifa ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya soka mwezi ujao kwa kufungwa na Barcelona bao 1-0.

Matangazo ya kibiashara

Kocha Jose Mourinho amesema licha ya kupoteza mchuano huo, amefurahishwa na maandalizi ya klabu yake kuelekea katika msimu mpya.

Bao pakee la Barcelona lilifungwa na mshambuliaji Neymar katika dakika ya 31 ya mchuano huo.

Barcelona walionekana kutawala mchezo huo hasa kipindi cha kwanza lakini, wakashindwa kutumia nafasi kadhaa walizopata kupata mabao zaidi.

Wachezaji wa Manchester United Anthony Martial, Paul Pogba na Andreas Pereira walijitahidi sana kujaribu kusawazisha bao lakini kipa Jasper Cillessen aliwanyima fursa hiyo.

Baada ya kucheza na Barcelona, Manchester United sasa itachuana na Valerenga ya Norway siku ya Jumapili kabla ya kumenyana na Sampdoria FC ya Italia katika mchuano wake wa mwisho siku ya Jumapili jijini Dublin.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.